Mahakama ya kijeshi nchini Misri imewahukumu watu thelathini na sita adhabu ya kifo kutokana na makosa ya mashambulizi dhidi ya makanisa ya Coptic.
Aidha, Watu sabini walikufa kutokana na shambulizi la bomu katika Kanisa Kuu la ki Coptic jijini Cairo mwishoni mwa mwaka 2016, na makanisa ya Alexandria na Tanta yaliripuliwa.
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu wenye msimamo mkali wamekiri kuhusika na mashambulizi hayo matatu, ambapo wamesema kuwa kazi yao kubwa ilikuwa kuwashambulia wakristo.
Hata hivyo, Misri inahitaji mahakama kupeleka kesi za namna hiyo kwa Mufti Mkuu nchini humo kwa kuzingatia adhabu ya kifo kabla ya hukumu ya mwisho.
-
Marekani kuchukua maamuzi magumu dhidi ya Syria
-
Msafara wa Mayweather washambuliwa kwa risasi.
-
Trump achukizwa na kitendo cha FBI kupekua ofisi za Cohen