Janga la tetemeko la Arhi lililoikumba mikoa ya Kanda ya Ziwa na kupelekea maafa ya watu 16 na majeruhi 253 limeibua mazito baada ya kubainika kuwa huenda lilishindwa kupimwa ipasavyo kutokana na kuimbwa kwa baadhi ya mashine za kupimia tetemeko la ardhi.

Hayo yamebainishwa na Mwanajiolojia, Gabriel Mbogoni aliyekuwa akizungumzia changamoto wanazokutana nazo katika kuhakikisha wanafuatilia na kubaini uwezekano wa kuwepo kwa matetemeko ya ardhi nchini.

Mbogoni alieleza kuwa kulikuwa na mitambo mitatu ambayo iliibwa na vituo vingine vidogo 38 vilisitisha kufanya kazi baada ya wafadhili kuondoka.

“Zamani tulikuwa tunatafuta maeneo yenye miamba migumu huko vijijini, tukipata tuanwasiliana na viongozi wa kijijini na tunaweka walinzi. Lakini zimeibwa, hali iliyopelekea tufunge vituo hivyo ,” Mbogoni anakaririwa na Mtanzania.

Aliongeza kuwa kutokana na wizi huo, waliamua kufunga mashine hizo katika maeneo ya Magereza kwa usalama zaidi isipokuwa katika vituo vya Mtwara na Dodoma.

Akieleza chanzo cha wizi huo, alisema kuwa ni tamaa ya watu wasio na nia njema ambao huzifananisha mashine hizo na madini.

Hata hivyo, alisema baada ya kuiba mashine hizo hushindwa kuzitumia wala kuziuza kwani zinautambulisho maalum na hazitumiwi kwa shunghuli nyingine.

Aidha, alisema kuwa hivi sasa vituo vikubwa vya kupimia matetemeko ya ardhi vipo katika maeneo ya Miko ya Mtwara, Dodoma, Geita, Arusha, Babati na Manyara.

Katika hatua nyingine, Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imesema kuwa itaanzisha program ya kutoa elimu kwa umma kuhusu namna ya kukabiliana na majanga kama matetemeko ya ardhi, kupitia vipindi vya TV na radio pamoja na machapisho mbalimbali.

Tetemeko lingine limeripotiwa kutokea jana katika maeneo ya mkoa wa Kagera jana lakini halikuzua madhara yoyote.

Rais Kenyatta, Mbowe watoa msaada kwa waathirika wa Tetemeko la Ardhi
Rais wa Ufilipino awafukuza wanajeshi wa Marekani akihofia balaa la ISIS