Zaidi ya waumini 2,000 wa Dini ya kiislamu kutoka ndani na nje ya nchi wamekusanyika jijini Dodoma wakilenga kukumbushana mambo Mbalimbali yanayohusu dini yao na mafundisho.
Kusanyiko hilo la siku tatu maarufu kama IJTIMAI, limekuwa na mada mbalimbali zikiwemo zilizochukua nafasi ambazo ni kulinda maadili na kumcha mwenyezi Mungu.
Awali, Katibu wa Bodi ya Wadhamini kutoka Taasisi ya Fiysabil lah Tabligh markaz ya Gongo la mboto Dar es Salaam, Sheikh Yahya Omary Mgeni , alisema mbali na Watanzania pia waislamu kutoka nchi za Afrika ya Mashariki walihudhuria
Hata hivyo, mkutano huo uliambatana na fursa Mbalimbali za maonesho ya Biashara, huku baadhi yao wakionekana kufurahia kile walichojifunza kama sehemu ya kuirudisha jamii katika mstari.