Asasi za Kiraia zimekutana hii leo Desemba 7, 2023 katika mdahalo wa kujadili jinsi ya kuimarisha nafasi ya Wanawake katika Uongozi Zanzibar.

Mdahalo huo pia umeangazia mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo, na njia za kufikia lengo la asilimia 50/50 kwenye nyadhifa za Uongozi.

Akiongea katika Mdahalo huo, Mkurugenzi wa TAMWA – ZNZ, Dkt. Mzuri Issa amesema lengo la kukutana kwao ni kuwashajihisha wanawake kugombea nafasi za uongozi.

“Lengo letu ni kuona jinsi gani wadau mbalimbali wanaweza kusaidia kuondoa vikwazo kwa wanawake katika uongozi ikiwemo viongozi wa dini, ZAECA na wengine,” amefafanua Dkt. Mzuri Issa.

Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Tone Tinnes ni miongoni mwa watu walioungana na wadau wa Asasi za Kiraia Zanzibar, kujadili nafasi hiyo ya Wanawake na Uongozi.

Singida Fountain Gate yafungiwa kusajili
Uongozi Mashujaa FC wakwepa shinikizo