Wajane zaidi ya kumi katika Kijiji cha Uchira wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamemwomba waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Wilium Lukuvi, kuingilia kati viwanja vyao walivyodhurumiwa na Jackson Chaky anayedaiwa kufanya kazi ya ulinzi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro akishirikiana na aliyekuwa Katibu Tarafa wa Vunjo Magharibi, Eskari Ndosi
Wajane hao wamesema kuwa wameshindwa kujenga nyumba kwenye maeneo yao hayo kutokana na kukosa makazi ya kudumu baada ya viwanja vyao kuvamiwa na Chaky ambaye anadaiwa pia kuwatishia maisha. Hivyo wameomba waziri Lukuvu kuwasaidia suala hilo nakuwachukulia hatua ili wapate haki zao.
Mmoja wajane hao, Zuleha Miraji amesema eneo lake ni lenye ukubwa wa nusu eka na kwamba anamiliki kihalali na ana nyaraka tangu mwaka 1986 ambayo ameachiwa na wazazi wake ambao wameshatangulia mbele za haki.
Polisi Tabora yawakamata 683
“Nina miaka zaidi ya 10 sijalima, kwani tayari eneo langu limeshauzwa kwa mtu mwingine na baada ya kufuatilia nimeambiwa hilo eneo limeuzwa na Chaky akishirikiana na Ndosi, na baada kumfuata Chaky alinitaka niondoke kwani sina haki yoyote pale.
“Chaky anatutishia maisha anatembea na panga sisi wajane tunamwongopa tunaiomba serikali ingilie kati tupewe haki zetu tunakwenda wapi, watu leo hii tumeshakuwa wazee hatuna uwezo wa kifedha wa kuendesha kesi maofisa ardhi hawaonyeshi ushirikiano jamani tunanyanyasika sana,” amesema.
James Mkojera ambaye ni shuhuda amesema maeneo ya wajane hao wananyaraka zote tangu mwaka 1986 akiwa kama shahidi, lakini cha kushangaza kuna watu wamejitokeza wanadai ni maeneo yao kinyume na taratibu za kijiji.
Akijibu tuhuma hizo, Jackson Chaky amesma hajawatishia maisha na kwamba anatembea na panga kwa ajili ya ulinzi wake binafsi.
Amesema, hao wanaomlalamikia kudhulumu maeneo yao wampelekee malalamiko hayo kwa maandishi.
“Panga langu hili huwa na beba kwa ajili ya shughuli zangu na ulinzi wangu binafsi,” amesema Chaky.