Wajasiriamali Mkoani Njombe wametakiwa kuzingatia kanuni za Kibiashara ikiwemo kulinda Mitaji yao ili kuhakikisha Mitaji inabaki salama bila kufilisika kutokana na Wajasiliamali wengi kufanyakazi bila kuzingatia kanuni za Kibiashara na Mwisho hujikuta wamefilisika.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la General Bussiness Company Limited, Alexander Malya alipokuwa akitoa Mafunzo ya Ujasiliamali wilayani Njombe kwa baadhi ya wakazi ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakishindwa kukua kutokana na Kutofuata kanuni za Kibiashara.

Amewataka wajasiliamali Mkoani Njombe kukuza Mitaji yao kwa kufuata kanuni za kibiashara huku akiwahimiza wananchi kutokuwa waoga kuomba mikopo katika taasisi mbalimbali za kifedha pamoja na kujiunga na mtandao wao wa kiuchumi kitaifa Unaofahamika kama fahari ili kujikwamua kiuchumi.

“Changamoto kubwa wananchi wetu wanapofeli vitu vingi tunafanya kwa mazoea hata maisaha yetu tunaenda nayo kwa mazoea, sasa biashara haifanywi kwa mazoea tunahitaji ifike mahala tuwaelimishe wananchi kufanya vitu kitaalamu na kufanya vitu kitaalamu ni lazima ubunifu utumike sana lazima tuwepo watu tunaoendana na uhitaji,”amesema Malya

Kwa upande wao, baadhi ya Wajasiliamali wadogo waliofika katika mafunzo hayo akiwemo diwani wa viti maalumu kata ya Njombe mjini, Anjela Mwangeni wameeleza umuhimu wa Mafunzo hayo huku wakieleza baadhi ya vikwazo yakiwemo masoko jinsi yanavyowarudisha nyuma.

 

Waandishi 38, wanaharakati kukamatwa kwa uchochezi mtandaoni
Kauli ya CAG yawakuna CCM, 'Acheni propaganda'