Siku moja baada ya mkutano huko Accra wa wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi – ECOWAS, ujumbe kutoka taasisi hii ndogo ya kikanda umekutana na Rais Niger aliyepindiliwa Julai 26, Mohamed Bazoum.

Ujumbe huo, uliwasili jiji la Niamey nchini Niger siku ya Jumamosi Agosti 19, 2023 na ulipokelewa uwanja wa ndege na Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Viongozi wa Mapinduzi, Mahamane Lamine Zeine wakiongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria, Abdulsalami Abubakar.

Mkutano huo ulifanyika mbele ya Waziri Mkuu huyo na mjumbe mwingine wa utawala huo wa kijeshi, na  hakuna habari iliyofichuliwa kuhusu mazungumzo yao, na inasemekana wajumbe wa ECOWAS walikuwa wamekuja kuona mazingira ambayo Rais aliyepinduliwa na kuzuiliwa anayoyaishi.

Awali, Viongozi hao walikutana na wajumbe wa serikali ya kijeshi, akiwemo Jenerali Tiani walikiwa na ujumbe wa kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kikatiba nchini Niger na kuomba mkutano mwingine na Rais wa zamani wa Niger, Mahamat Issoufou.

Mashirika 28 kuachana na utegemezi Serikalini
Mashirika ya umma yawauzie hisa Wananchi - Rais Samia