Wizara ya Viwanda na Biashara imewajengea uwezo wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi la Kilimo, Biashara na Utalii kuhusu Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCTA).

Wajumbe hao wamejengewa uwezo huo kupitia semina iliyowakutanisha wajumbe wa kamati hizo iliyofanyika Novemba 12, 2021 Jijini Dodoma ikiwa ni hatua ya Wizara katika kutekeleza mkakati wa kujenga uwelewa wadau kuhusu mkataba huo.

Aidha, katika nyakati tofauti wajumbe wa Kamati hizo wametoa maoni na kutaka wafanyabiashara kuchangamkia fursa za biashara wakati wa kutekeleza mkataba huo utakapoanza ikiwemo uondoaji wa viwakzo vya kibiashara, uzalishaji wa bidhaa zenye ubora, usafirishaji wa bidhaa, kodi, na sheria mbalimbali zinazohusika na biashara pamoja na kuzingatia, kulinda na kuweka maslahi ya Taifa mbele wakati wote wa utekelezaji wa mkataba huo.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (MB), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema Serikali imejiandaa kikamilifu katika kutekeleza Mkataba huo ambao utachangia kukua kwa uchumi hapa nchini.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Biashara na Utalii ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Yussuf Hassan Idd ametoa rai kwa Serikali kujipanga kutumia fursa zinazopatikana kutokana na maktaba huo huku ikizingatia utofauti wa uchumi kati ya nchi wananchama wa bara la Afrika wanaotekeleza mkataba huo.

Awali akimkaribisha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Tax, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Doto James amesema Tanzania imeridhia na Mkataba huo ambao unafaida nyingi kwa taifa ikiwemo upatikanaji wa soko kubwa la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takriban bilioni 1.2.na utasaidia kuongezeka kwa tija na ubora kwa bidhaa na huduma za Tanzania kutokana na kuongeza kwa ushindani na hivyo kupelekea kupungua kwa bei za bidhaa

Jafo atoa maagizo kwa wakuu wa Mikoa,Wilaya,Halmashauri
Kuvumilia sana chanzo cha uraibu