Naibu Makamu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro, Prof. Mussa Assad amesema Wajumbe wa Bodi katika Taasisi za Umma wanatakiwa kupatikana kwa utaratibu wa usaili, ili kupata viongozi watakao ongeza tija kwa taasisi.

Prof. Assad ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma uliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano jijini Arusha, AICC.

Amesema, “upatikanaji wa wajumbe wa bodi ni muhimu ili kuwa na usimamizi thabiti wa mashirika hayo na ukifanya usaili utachuja kwani Wajumbe wa bodi wanapaswa kufanyiwa usaili, usipofanya hivyo unajikuta una wenyeviti wa bodi wa tangu miaka ya 60.”

Prof. Assad ambaye aliwahi kuwa Mkaguzi Mkuu wa zamani wa Hesabu za Serikali, amesema uwepo wa bodi ni muhimu kwani unawezesha uwepo wa usimamizi mzuri wa rasilimali za taasisi.

Wafariki kwa kutumbukia shimoni wakiwa harusini
Mashirika 28 kuachana na utegemezi Serikalini