Afara Suleiman, Babati – Manyara.

Wakaguzi wa Polisi Mkoani Manyara, wametakiwa kuzingatia Haki na Weledi katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Wito huo, umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi wakati akifunga Mafunzo ya utayari ya kuwajengea uwezo askari Polisi kada ya wakaguzi na wakaguzi wasaidizi awamu ya lll yaliyohitimishwa hii leo Novemba 3, 2023.

Amesema, Wakaguzi hao wanatakiwa kuyatumia Mafunzo hayo kujibadilisha kifikra kwa kuongeza ukakamavu na kujiamini wakati wakitekeleza majukumu yao na kuwataka kufanya kazi kwa kujiamini na kwa kuzingatia Sheria na kanuni za Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi katika kuzuia, kubaini na kutanzua uhalifu na wahalifu.

Kamanda Katabazi, pia amewataka wakaguzi hao kuwa mabalozi wazuri katika Kata zao kwa kuielimisha juu ya miradi ya Polisi Jamii na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto hususani ukatili wa kingono na kutojichukulia sheria mkononi.

Mafunzo hayo ya utayari awamu ya III, yamefanyika katika Mkoa Manyara kwenye wilaya za Babati, Simanjiro, Kiteto, Hanang’ na Mbulu.

Polisi Katavi wabaini uhalifu wa Bajaji
Hassan Dilunga afunguka kwa uchungu