Chelsea ilifikia makubaliano binafsi na Mohammed Kudus kabla ya uhamisho wake wa Pauni Milioni 38 kwenda West Ham majira ya joto, na hiyo ni kutokana na ofa ndogo iliyotolewa kwa Ajax, wakala wa mchezaji huyo amethibitisha.
The Blues ilianza msimu mwingine wa matumizi makubwa ya fedha kwenye uhamisho, kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwa Moises Caicedo, Romeo Lavia, Nicolas Jackson, Christopher Nkunku, Axel Disasi na Cole Palmer
Kudus alikuwa akivutiwa na Manchester United, baada ya kufanya kazi na Erik ten Hag kule Ajax, na Arsenal, lakini, Chelsea walikuwa wa kwanza kufanya mazungumzo na kambi ya mchezaji huyo.
Katika mwonekano wake kwenye kituo cha redio cha RMC, wakala, Jen Mendelewitsch alizungumzia nia ya Chelsea kwa mteja wake, na kusema mambo yaliharibilka dakika za mwisho kwa Ajax kukataa ofa iliyowekwa mezani.
“Chelsea ilikubaliana maslahi binafsi na Kudus,” alieleza, kabla pia kufichua The Blues “walipunguza ofa” kwa Ajax kuwa Pauni Milioni 175.
Kulikuwa na kidokezo cha juhudi za muda mrefu za kujaribu kumsajili Caicedo, ambazo Chelsea ilifanya kwa Pauni Milioni 115, zilikuwa ngumu sana.
“Ukweli Chelsea walichukuliwa kabisa na uhamisho wa Caicedo, ambao ulichukua nguvu zao zote,” alisema Mendelewitsch.
Kudus alijiunga na Ajax kutoka Nordsjaelland ya Denmark mwaka 2020 muda mfupi kabla ya kufikisha umri wa miaka 20, ingawa haikuwa hadi msimu uliopita ambapo alijiunga na klabu hiyo ya Amsterdam na kujitangaza.
Alifunga mabao 18 katika mashindano yote wakati wa msimu huo, ikiwa ni pamoja na manne katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Tangu atue West Ham, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, amefunga mara mbili katika mechi nane kwenye michuano yote, lakini bado hajaanza mechi ya Ligi Kuu England.