Rapa Wakazi ambaye pia ni meneja wa Lady Jay Dee, ametajwa kuwania tuzo za Kora mwaka huu katika kipengele cha rapa bora  ‘Best Hip Hop Act’. Tuzo hizo zitatolewa Windhoek, Namibia mwezi Machi mwaka 2016.

Wakazi ambaye ni rapa anaependa kuwakilisha eneo la Ukonga jijini Dar es Salaam kama hood yake ya ‘kujidaia’, ametajwa katika kipengele hicho akiwa na rapa wakubwa Afrika ambao ni K.O (Afrika Kusini), Sarkodie (Ghana), Stanley Enow (Cameroon), Hamzaoui Med Amine (Tunisia) na Kiff No Beat (Ivory Coast).

Kora

Kupitia Instagram, Wakazi ameandika:

“I have received with greatest shock & joy (almost crying) the news of being nominated for the 2016 @kora_awards “BEST HIP HOP ACT”. All I ever wanted is to be recognized & appreciated for the work I put out. A nomination is already a win for me… Let’s celebrate this together first before we start the strategy of voting for the win. This is for TZ Hip Hop & all upcoming artists with a dream to make it.”

Lupita Nyong’o ‘Achemsha’ Kwenye Filamu Ya Star Wars, Muongozaji Ashindwa Kuvumilia
‘Ander Herrera, Marouane Fellaini lazima Waondoke Old Trafford’