Rapa Wakazi ameibuka na jipya kuhusu kujitoa kwenye tuzo za muziki kwa msanii Nay wa mitego ambaye hivi karibuni alitangaza kujiengua kutokana na kile alichodai kuwa hajaridhishwa na mwenendo mzima wa maandalizi na uendeshwaji wa tuzo hizo.
Wakazi amedhihirisha kuheshimu maamuzi ya Nay, huku akikosoa kitendo cha kujitoa kwenye tuzo hizo hali ya kuwa suala la uwepo wa tuzo kwenye kiwanda cha muziki Tanzania kilikuwa kilio cha muda mrefu na uamuzi wa serikali kuzirejesha ni wa busara licha ya uwepo wa udhaifu kwenye maeneo kadhaa.
Rapa huyo amegusia kuwa wasanii kuendelea kuwepo ndani ya tuzo na kuziunga mkono badala ya kujiengua kutachangia urahisi wa kufanyiwa kazi kwa changamoto hizo ili kuleta mabadiliko chanya kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini.
“Miaka 8 hamna Tuzo nchini, alafu tukawa tunajidanganya “Muziki wetu umekua,” Nchi ambazo Muziki ni mkubwa au umekua, kuna Tuzo 20 kidogo. There was a dire need to brick back these Awards. (Wizara, Waziri Bashungwa, Waziri Mchengerwa, Katibu Mkuu Dkt Abbasi, Cosota, Basata na Watendaji wake wanastahili pongeza kwa hatua hii) But let’s get realistic kidogo.” Aliandika Wakazi.
Aidha ameendelea kuandika kwa kuhoji na kujijibu, “Kurudi kwa Tuzo ni kitu cha msingi sana? bila shaka. Tuzo zina mapungufu? haipingiki. Waandaaji wamejitahidi kupokea mawazo ya uboreshaji? without a doubt. Kuna baadhi ya Mapungufu ni ya kizembe? absolutely. Kuna baadhi ya Mapungufu yanaweza rekebishika kwa sasa? Bila shaka. Kuna makosa mengine ya kiufundi yanahitaji kusubiria mwakani? Kabisa. Wasanii tunahitaji kuzisupport Tuzo? yes indeed.”
Aidha rapa huyo ametaja manufaa zaidi ya wasanii wote kwa pamoja kushikamana katika kuziunga mkono tuzo hizo zitolewazo na Serikali kupitia Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo chini ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) na kutoa rai kwa wasanii wengine waliozipuuzia tuzo hizo.
“Vitu visipokaa sawa, alafu wewe unaona kabisa vingeweza kukaa kama wangekuwa makini kidogo, huwa ina frustrate. Ndio maana ninamuelewa Nay Wa Mitego kwa maamuzi aliyochukua. Ila upande wa pili, uwepo wa Tuzo ni muhimu zaidi.
So badala ya kuzisusia na kufanya pengine ziondoke tena, ni bora kushiriki na kuendelea kudai maboresho as we go. Hii sio tu kwa Nay, ila na baadhi ya wasanii wengine ambao walisusia kushiriki. Tuweke Muziki, Sanaa mbele na sio maslahi yetu binafsi.” Wakazi.
Wakazi ameyasema hayo kupitia maelezo aliyoyavhapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram mapema Machi 30, 2022.