Wakazi wa Kata ya Ilembo Halmashauri ya Wilaya Mbeya, wameipongeza Serikali kwa kufanikisha kufikisha huduma ya Umeme na Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Pareto, hali inayoonesha nia ya dhati ya Serikali kusogeza Maendeleo katika Vijiji vilivyopo ndani ya Kata hiyo.

Pongezi hizo, zimetolewa mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa kutembelea Katika kata hiyo Ili kujionea Maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Wasichana Pareto na kusikiliza kero za Wananchi wa kata hiyo ambapo Wananchi waliibuka na kutoa hisia zao juu ya kile kilichofanywa na Serikali katika kusogeza Miundombinu ya Umeme ambapo kwa muda mrefu vijiji hivyo vilikosa huduma hiyo.

Wamesema, Serikali imefanya jambo muhimu kuwashirikisha wadau ili kusaidia Ujenzi wa Shule ya wasichana itakayosaidia wasichana waliopo katika kata hiyo kutotembea umbali mrefu kufuta huduma ya elimu.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Kwa Upende wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, amewasisitiza Wakazi wa Ilembo na Halmashauri ya Wilaya Mbeya kushirikiana ipasavyo na Makampuni yanayojihusha ununuzi wa zao la Pareto ambao waliahidi kuchangia ujenzi wa Shule hiyo, haraka iwezekanavyo.

Aidha, Malisa ameendelea kuwasisitiza Wakazi wa Ilembo kuwa wavumilivu kwa maana Serikali yao ni Sikivu na itendelea kuwapelekea maendeleo katika maeneo hayo, ikiwemo kuboresha Miundombinu ya Barabara na Maji.

Dkt. Biteko azindua mkakati kutangaza fursa za Utalii
Mgogoro ukanda wa Gaza washika kasi