Wakazi wa kijiji cha Itengelo Kata ya Saja Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe wamelalamikia uwepo wa dampo juu ya milima ambalo linadaiwa kutiririsha maji machafu kwenye vyanzo vya maji na hivyo kusababisha magonjwa ya mlipuko.
 
Wakizungumza mwishoni mwa wiki wakazi hao wamewaomba wataalamu wa mazingira kwenda kuangalia athari zinazowakabili wakazi hao na hivyo kushawishi serikali za wilaya hiyo na wilaya ya Njombe kuliondoa dampo hilo.
 
Wamesema kuwa kipindi cha mvua za masika wamekuwa wakikumbwa na magonjwa ya tumbo na kuhara kutokana na kutumia maji katika vyanzo ambavyo hupokea maji machafu pamoja na takataka yanayotoka katika dampo hilo.
 
‘’Dampo hili linatumiwa na halmashauri ya Makambako na si Wanging’ombe na limekuwa katika mgogoro kuhusu eneo lililopo kwa muda mrefu na waathirika sio Njombe ni sisi, tumekuwa tukipata magonjwa ya matumbo pamoja na kuhara yanayosababishwa na kunywa maji yanayotoka katika vyanzo na hii inatokana na dampo kuwa juu ya mlima hivyo uchafu wote unashuka katika hivi vyanzo vya maji’’amesema Mohamed Kimata.
 
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Itengelo, Jairos Mwinulile amekiri kuwepo kwa malalamiko ya athari hizo za magonjwa ya tumbo na kuhara na hivyo kupelekea kupunguza uzalishaji kwenye shughuli zao za kilimo.
 
  • Huwezi kuwaita Wabunge wa CCM ‘Makasuku’- Lusinde
  • Shule iliyoathiriwa na bomu Kagera yapata msaada
  • Wizara ya Maliasili na Utalii yazigeukia Fukwe
 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Saja, Andrew Mangula amesema kuwa jitihada mbalimbali zimefanyika ikiwemo kuzungumzia changamoto hiyo katika vikao vya baraza la madiwani bila ya mafanikio

Sekretarieti ya Ajira yatakiwa kutenda haki
Kabila lenye lugha ya zamani kuliko makabila yote duniani