Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbulu, limewataka Wananchi kuwafichua watuhumiwa wa Ukatili wa Kijinsia, ikiwemo wanaowapa mimba Wanafunzi na kuwakeketa, ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya Sheria.

Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto Polisi Wilayani humo, Sajenti Glory Daudi ametoa witi huo wakati akitoa elimu ya kupinga Ukatili wa Kijinsia katika Shule ya Sekondari Singland na Shule za Msingi za Harka na Waama.

Amesema, Wanafunzi ni kundi kubwa katika jamii hivyo wakishirikishwa katika mapambano ya kupinga vitendo hivyo watakuwa na mchango mkubwa na kulirahisishia Dawati la Jinsia kupata taarifa za ukatili ili kuchukua hatua huku akiwatahadharisha kutoshiriki michezo hatarishi.

Aidha, Sajenti Glory amebainisha kuwa “kesi za ukatili zisimalizwe nyumbani kienyeji na ndugu bali zifikishwe Polisi ili mtuhumiwa afikishwe mahakamani na msisite kutoa ushahidi, msimalizane kienyeji, leteni taarifa kwenye Dawati watashughulikiwa.”

Ukatili wa Kiuchumi na Kingono hususani ngono kwa watoto imekuwa ikikemewa na Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Wilayani humo na tayari wamefanikiwa kufikisha elimu kwa makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo Wanafunzi wa Sekondari na shule za Msingi.

Newcastle United kutupa ndoano Saudi Arabia
Kocha Wydad Casablanca aomba radhi