Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata, leo Ijumaa April 24, 2020 ametangaza kuwarudisha wakenya waliopo nchini China katika Jiji la Guanzhou mnamo mei 1, mwaka huu.
Akitangaza uamuzi huo, Rais Kenyata amesema Serikali ya nchi hiyo itatuma ndege ya shirika la Kenya Airways kwaajili ya kuwarudisha wakenya waliopo nchini china ambao wameomba kurudishwa nchini kwao.
Naye Balozi wa Kenya kutoka China, Sarah Serem amesema hatua hiyo inafuata baada ya maombi ya Wakenya wengi waliopo China ambao walipaza sauti ya kubaguliwa na wenyeji na kuiomba Serikali ya nchi yao kuwarudisha nyumbani.
“Serikali ya Kenya imetoa ndege itakayowarudisha nyumbani wakenya wote ambapo nauli imepunguzwa mpaka Ksh 80,000 kwa daraja la ‘economy’ kuwawezesha wakenya watakaotaka kurudi nyumbani kumudu gharama za usafiri” amesema Balozi Serem.