Wakili maarufu na Mwanasiasa ambaye aliwahi kuwa  Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mmoja wana familia zinasema Nimrod  amefariki asubuhi ya leo (Aprili 18, 2023) nchini Marekani kwa matibabu.

Alikuwa akikabiliwa na  tatizo la kusahau, (kupoteza kumbukumbu),na taarifa juu ya taratibu nzima na mazishi zitatolewa hapo baadaye.

Nimrod Elirehemah Mkono, alizaliwa Agosti 18, 1943 katika Kijiji cha Busegwe na alikuwa ni Mbunge wa Musoma Vijijini tangu mwaka 2000 – 2015.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Aprili 19, 2023
Halmashauri zakumbushwa matibabu bure kwa Wazee, wasiojiweza