Katika kuhakikisha kikosi cha Namungo FC kinakua na makali kwenye michuano ya Kombe la Shiriksho Barani Afrika, kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleyman Morocco amedhamiria kufanya usajili wa mchezaji anayecheza nafasi ya ushambuliaji.

Morocco ambaye tangu alipojiunga na Namungo FC amekua na matokeo mazuri, amesema mchezaji anayedhamiria kumuongeza kikosini kwake, atakua wakimataifa.

Amesema mpango wa kufanya usajili huo, unatokana na hali ya mshambuliaji wake mzawa Adam Salamba ambaye kwa muda mrefu amekua nje ya kikosi cha Namjungo FC, kufuaria majereha yanayomkabili.

“Ninahitaji kuongeza mshambuliaji hasa ukizingatia kwamba mchezaji wetu mmoja bado anasumbuliwa na majeraha na hajarejea kwenye ubora.”

“Adam Salamba bado hayupo fiti hivyo ni wakati wetu kuingia sokoni kusaka mshambuliaji ambaye tutakuwa naye ndani ya kikosi kwani mbali na ligi tunashiriki mashindano ya kimataifa.” Amesema Morocco

 Namungo FC jana Jumapili (Desemba 27) ilitinga hatua ya nne ya Kombe la Shirikisho (ASFC) baada ya kushinda mabao mawili kwa moja  dhidi ya Green Warriors kwenye mchezo wa hatua ya tatu uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Mabao ya Namungo yalipachikwa na Idd Kipagwile kwa mpira wa adhabu nje ya 18 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa faulo ilikuwa dakika ya 8 kwa pigo huru na Sixtus Sabilo dakika 78.

Katika hatua nyingine Namungo FC ina kazi ya kusaka ushindi ugenini dhidi ya Al Hilal Obeid ya Sudan kwenye michuano ya Kombe la Shiriksho Barani Afrika, baada ya kuibuka kidedea kwa mabao mawili kwa sifuri kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Desemba 23.

Mchezo wa mkondo wa pili umepangwa kuchezwa mjini Khartoum, Sudan kati ya Januari 5-6 nchini Sudan.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 29, 2020
Wananchi Nzega watoa kongole kwa Airtel

Comments

comments