Wakimbizi watano kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamefariki na wengine 20 kujeruhiwa nchini Rwanda katika maandamano ya kupinga punguzo la lesheni ya chakula inayotolewa na Umoja wa Mataifa.
Zaidi ya wakimbizi 3,000 waliweka kambi katika ofisi za Umoja wa Mataifa nchini humo kwa siku mbili wiki iliyopita, ambapo siku ya Alhamisi Jeshi la Polisi lililazimika kuwatawanya kwa mabomu ya machozi.
Msemaji wa Jeshi hilo, Theos Badege aliviambia vyombo vya habari kuwa wakimbizi hao walifanya fujo na kuwarushia askari mawe na vitu vingine yabisi.
“Walianza kurusha mawe, vipande vya vyuma… wakimbizi 20 walijeruhiwa, askari wa jeshi la polisi saba walijeruhiwa pia. Katika tukio hilo, wakimbizi watano walipoteza maisha,” alisema Badege.
- Video: Wanasheria wahaha kumnusuru Sugu, Mbowe atoa kauli nzito mazishi ya Diwani Luena
- Jeshi na Polisi watofautiana nchini Nigeria
Kupitia akaunti ya Twitter ya jeshi hilo, imeelezwa kuwa wakimbizi 15 walikamatwa. Jeshi hilo linaleza kuwa kuwa idadi ya waandamanaji ilikuwa 500 huku Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi likieleza kuwa walikuwa waandamaji 700.
Wakimbizi hao wanapinga uamuzi wa Umoja wa Taifa kupunguza lesheni ya chakula kwa asilimia 25.