Abel Paul – Jeshi la Polisi, Dar es Salaam.
Timu ta mpira wa Pete kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) imeibuka na ushindi wa magoli 19 kwa 4 dhidi ya timu ya mpira wa Pete ya wakaguzi wanafunzi katika mashindano ya Polisi jamii Cup.
Awali matroni wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) Mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP Anitha Semwano aliwataka wachezaji hao kuonyesha ujuzi na mbinu za kimchezo ili kupata ushindi dhidi ya timu pinzani katika mashindano hayo yaliyofanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam yenye lengo la kuwaleta karibu wananchi na Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake mrakibu msaidizi wa Polisi ASP Rose Haule amesema matokeo mazuri walioyapata yametokana na maandalizi mazuri waliyoyafanya ambapo imepelekea ushindi huo.
Nae mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msaidizi wa Polisi Rizi Fred amesema mbali na kupata matokeo hayo ambayo sio mazuri kwao, amewaahidi kuwa wanajipanga upya kwa ajili ya mashindano yajayo ambapo amewahidi mashabiki kuwa watafanya vizuri Zaidi.
Mchambuzi wa Mchezo huo ambae ni mwanafunzi wa kozi ya uofisa Christer Kayombo amesema kuwa timu ya wakaguzi walionekana wako vizuri kipindi cha kwanza cha mchezo lakini timu ya wakufunzi walitumia madhaifu yao kubadilisha mchezo na hatimae timu ya wakufunzi iliibuka na ushindi.
Sambamba na hilo Umefanyika mchezo wa riadha wa kukimbia mita mia moja na mita mia mbili ya kupokezana vijiti ambapo mshindi wa mita mia moja alitoka katika timu ya wakufunzi wa chuo hicho mrakibu msaidizi wa Polisi ASP Grace Makazi.
Pia katika mbio za kupokezana vijiti kombania C wameibuka na ushindi katika mashinda hayo ambapo mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msadizi wa Polisi Emmanuel Semfukwe amesema ushindi wao umechagizwa na mazoezi wanayofanya kila kila siku kitendo kilichopelekea ushindi wa jumla katika mbio hizo.