Watu sita wameuawa  na wengine saba kujeruhiwa katika kijiji cha Ngongo Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana, Novemba 12, 2019.

Mauaji hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, amesema watanzania sita walipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kutoka nchi jirani ya Msumbiji wakati wakiwa katika visiwa vya mto Ruvuma wakiendelea na shughulizao za kilimo.

“Usiku walivamiwa na kikundi cha watu waliowakusanya pamoja na kuwapiga risasi. watu sita walifariki dunia na wengine saba waliojeruhiwa wamelazwa katika Hospitali ya Tandahimba” amesema DCI Boaz.

Ameongeza kuwa ” Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya dola tunachukua hatua madhubuti kuhakikisha wote waliohusika na tukio hili wanapatikana na kuchukuliwa hatua”

Na amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi na kuwataka wananchi kuchukua tahadhali wanapokwenda nchi nyingine kufanya shughuli za kiuchumi.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 14, 2019
Majeraha yamharibia Mo Salah kwa Kenya