Wakulima mkoani Njombe wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea ili kuboresha Sekta ya Kilimo mkoani humo na kufikia malengo makubwa ya Kiuchumi kwa kuzalisha mazao ya kibiashara.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe, Erasto Ngole ambaye ni mkulima mkubwa wa zao la Parachichi na Mbogamboga mkoani humo.

Amesema kuwa mti wa Parachichi licha ya kutoa matunda ambayo yanasoko kubwa ndani na nje ya nchi, pia mmea huo ni Tiba kwa mwili wa Binadamu.

“Watanzania tuwe na tabia ya kuwalisha watoto wetu vyakula vya asili ili waweze kuwa na afya bora ambayo itawakinga na magonjwa mbalimbali,”amesema Ngole

Aidha, amesema kuwa baada ya kuzalisha zao hilo, kwasasa ameamua kuongeza kilimo kingine cha mbogaboga ikiwemo Kabeji na Maharage kwa wingi.

Hata hivyo, baadhi ya Wakulima katika maeneo tofauti mkoani Njombe wamemuelezea Ngole kuwa kama mfano wa kuigwa na wakulima wote nchini.

 

Meya wa mji wa Njombe awacharukia wakazi wa mjini kuhusu michango
Video: Mwijaku achambua kilio cha MCPilipili , ‘aliwahi kuniambia...’