Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Wakulima wa Alizeti katika Vijiji sita vilivyopo Wilayani Babati Mkoani Manyara, wametakiwa kuongeza thamani ya zao hilo kwa kulichakata na kuuza mafuta ya kula pamoja na mabaki yanayotumika kulisha mifugo badala ya kuuza alizeti ghafi zikiwa shambani kwa bei ya chini.

Wito huo, umetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la COSITA, Patrice Gwasma huku wanufaika wa mradi huo baada ya kupatiwa elimu ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ikiwemo alizeti, wakisema watachangamkia fursa hiyo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kujiongezea kipato.

Awali, Mratibu wa Mradi wa Haki za Wanawake katika mazao ya kilimo na ufugaji kutoka shirika la COSITA alisema upo umuhimu wa Wakulima hao kuongeza thamani katika mazao ya alizeti na kuwataka  kusindika mazao yao kabla ya kuyapeleka sokoni .

Kwa upande wao Viongozi wa Vijiji vya Wilaya ya Babati ambao pia ni wakulima  na wanufaika wa mradi wamesema baada ya kupata elimu hiyo, wataanza kukamua na kusindika mazao yao ili kuyapa thamani.

Bangala, Fei Toto waipa jeuri Azam FC
Ahmed Ally atuma salamu Ligi Kuu 2023/24