Mkuu wa kituo cha Polisi Dumila, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ASP Emamanuel Mabembere ametoa elimu kwa wafugaji wa kijiji cha Msowelo kata ya Msowelo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro juu ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwenye kata hiyo.
Elimu hiyo, imetolewa na ASP Mabembere hii leo Septemba 20, 2023 ambapo amewataka kutambua wao wanategemeana kwani Mkulima huhitaji Nyama na Maziwa huku Mfugaji naye akihijaji chakula.
Amesema, “kitendo cha Mfugaji kumuuzia nyama na maziwa mkulima na kitendo cha mkulima kumuuzia vyakula mfugaji ni ishara tosha kuwa jamii hizi mbili zinaishi kwa kutegemeana. Kwa hivyo basi inatupaswa kuheshimiana na kushirikiana na sio kugombana.”
Aidha, ASP Mabembere pia aliwaelimisha umuhimu wa kuwa na Mazizi salama pamoja na maeneo maalumu ya kuchungia, ili kuepusha kulisha maeneo ya mashamabani pamoja na umuhimu wa kutunza Mazingira.