Wakulima wa zao la korosho wa wilaya ya Newala na Tandaimba wamekataa kuuza korosho mbele ya Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba, kutokana na kushuka kwa bei ya zao hilo.
Hayo yamejiri kwenye mnada wa kwanza wa msimu wa uuzaji korosho 2018/2019 ulio jumuisha kampuni za ununuzi 17 uliofanyika katika kijiji cha Makukwe wilayani Newala mkoani Mtwara.
Wakulima hao walifikia uamuzI huo baada ya kushtushwa na na bei za wanunuzi wa zao hilo kutokidhi gharama za uzalishaji wa zao lao, mmoja wa wakulima hao khamis Juma amesema kuwa nibora wazibangue wenyewe waziuze polepole kuliko kuwapa wanunuzi hao ambao wame enda wakiwa tayari wameshauriana bei zao ambazo zinakinzana na zawakulima.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Mtwara ameungana na wakulima kupinga bei hizo na wakuwataka wananchi wa mtwara wote kuungana pamoja kuzikataa bei za unyonyaji na serikali itawaunga mkono kwa nguvu zote.
Na kwa upande wake Naibu Waziri wa kilimo, Omary Mgumba aliwataka wakulima wa mazo mengine ya biashara kuzingatia ubora kwani kumekuwa na tabia ya mazao yote ya biashara kukosa sifa ya ubora, na kuonya kuwa serikali ya awamu ya tano haita mvumilia mkulima yeyote wa zao la biashara ambalo litakosa sifa, itamchukulia hatua kali na kumuingiza kwenye makosa ya uhujumu uchumi.