Wakulima katika Skimu ya Umwagiliaji ya Lemkuna iliyopo katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, wameiomba serikali kuwaongeazea eneo linalotumika katika kilimo cha umwagiliaji kwa sasa lenye ukubwa wa Hekta mia tatu (300) mbali na zaidi ya hekta elfu kumi (10,000) zilizoendelezwa kwa kilimo cha hicho.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha wakuliwa Lemkuna Uwale, Stanley Msuya amesema kuwa kutokana na kilimo hicho kuwa na mafaniko na faida kubwa katika jamii inayozunguka maeneo jirani, kumekuwa na mwamko mkubwa wa vijana wa kujiajiri kupitia sekta ya kilimo, lakini maeneo mengi yamekuwa yakimilikiwa na watangulizi au wazazi wao jambo ambalo limepelekea vijana hao kukosa maeneo ya kufanya shunguli za kilimo.
“kilimo hiki cha umwagiliaji kimekuwa na faida kubwa kwetu sisi wakulima hasa baada ya serikali kupitia tume ya Taifa ya Umwagiliaji kutujengea miundombinu ya umwagialia, kipato cha mkulima mmoja kabla ya maboresho na kupatiwa mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji, mkulima aliweza kupata gunia za Mpunga kwa mfano kuanzia kumi na tano (15) mpaka ishirini (20) kwa heka moja, lakini kwasasa mkulima anaweza kupata gunia thelathini na tano (35) mpaka hamsini (50) unaweza kuona namna ambavyo kilimo hiki kina faida, Hivyo tunaiomba serikali kufanya upanuzi wa eneo hili kwani vijana wanahitaji sana kufanya shughuli za kilimo.” amesema Msuya.
Aidha, Msuya amezitaja baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo kuwa ni pamoja na Chama hicho kukosa vifaa vya kuvunia zao la mpunga na ili kukabiliana na changamoto hiyo kipo kwenye mchakato wa kupata mkopo kupitia Bank ya kilimo na Bank ya NMB nchini ili kuweza kununua mashine hiyo na kuweza kuinua wakulima wadogo wadogo kwa kuchangia katika upatikanaji wa pembejeo za kilimo na kuongeza mtaji.
-
Wakulima waiomba serikali kuwaongezea eneo la kilimo cha umwagiliaji
-
Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro yanufaika na Kilimo cha Umwagiliaji
-
TFDA yaja na mfumo mpya wa udhibiti usalama wa Chakula
Skimu ya kilimo cha umwagiliaji Lemkuna ipo katika kanda ya umwagiliaji ya Dodoma, inayohusisha mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara.