Mahakama ya Ubelgiji, imewakuta na hatia watu 10 waliotoa msaada kwa kundi la kigaidi la Kiislamu (Islamic State), lililoua watu 130 ndani na nje ya jiji la Paris mwaka 2015.
Hukumu hiyo, imetolewa ikiwa ni siku moja baada ya wanaume 20 kukutwa na hatia jijini Paris kutokana na kuhusika katika mashambulizi hayo ya mfululizo wa risasi na milipuko ya kujitoa mhanga.
Mashabulizi hayo yanadaiwa kufanyika katika ukumbi wa tamasha wa Bataclan, uliopo eneo la nje ya uwanja wa Taifa wa soka wa nchini Ufaransa na kwenye matuta ya midahawa iliyopo katikati ya jiji la Paris.
Washtakiwa hao raia wa Ubelgiji (wanaume 13 na mwanamke mmoja) sambamba na wengine wawili wali0shtakiwa bila kuwepo hawakushtakiwa nchini Ufaransa kwa sababu walishukiwa kuwa na majukumu na wanakabiliwa na mashtaka madogo.
Mmoja wa washukiwa wakuu, Abid Aberkane alipatikana na hatia ya kumpa hifadhi Salah Abdeslam ambaye ni binamu yake na mwanachama pekee aliyenusurika wa timu iliyoendesha mashambulizi ya Paris.
Mashambulizi ya Paris na Brussels yalifichua kushindwa kwa Uropa kushiriki taarifa za kijasusi, kulinda mipaka na kushughulikia mchanganyiko hatari wa uhalifu na itikadi kali katika vitongoji vya wahamiaji waliokata tamaa ambapo Waislam wenye msimamo mkali walivamia.
Mtandao wa Islamic State, ambao ulifanya mashambulizi ya Paris pia ulishambulia Ubelgiji baadaye Machi 2016 kwa milipuko ya kujitoa mhanga katika uwanja wa ndege wa Brussels na katika metro ya jiji hilo ambayo iliua watu 32.
Wanaume kumi wanaotuhumiwa kuhusika na mashambulizi ya Brussels wamepangwa kuhukumiwa Oktoba, 2022, wakiwemo wachache waliopatikana na hatia mjini Paris siku ya Juni 29, 2022.