Tetemeko la Ardhi lililoikumba Kanda ya Ziwa jana limeacha maafa, majeruhi na uharibifu mkubwa wa mali za wakazi wa mikoa ya Kagera, Mwanza na Mara.

Tetemeko hilo limeripotiwa kuwa na madhara makubwa zaidi katika Mkoa wa Kagera ampabo watu 10 wamethibitika kupoteza maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamethibitisha vifo vya watu 10, majeruhi 100 pamoja na nyumba 40 kubomolewa na tetemeko hilo.

tetemeko-2

Aidha, mikoa mingine ya Kanda ya ziwa ambayo pia ilikubwa na tetemeko hilo, haikupata madhara makubwa na hakuna vifo vilivyothibitishwa kutokea.

Wakuu wa Mikoa ya Mara, Mwanza na Geita kwa nyakati tofauti walisema kuwa walipata taarifa ya tetemeko katika mikoa yao ambalo lilidumu kwa dakika chache lakini hakukuwa na taarifa yoyote ya vifo na majeruhi.

Mamlaka ya Hali ya Hewa imesema kuwa inaendelea kufanya uchunguzi wa kina kujua madhara yaliyotokana na tetemeko hilo.

“Tunafuatilia kujua ukubwa wa skeli ya Richter na tujue kama limeweza kuathiri kwa kiasi gani,” Ofisa wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mkoa wa Mwaza anakaririwa.

Kufuatia tukio hilo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli alimtumia salam za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Ollomi akieleza kushtushwa na janga hilo lililochukua uhai wa wananchi.

 

Chukua hii: Lipumba alitaka Jaji Warioba agombee Urais kupitia Ukawa, Sio Lowassa
Kocha Mkuu Simba Joseph Omog Aipa Ubingwa Yanga Msimu Huu