Baada ya kubaini kuwa uchaguzi wa marudio Zanzibar hauzuiliki na utafanyika kama ilivyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, Chama Cha Wananchi (CUF) kimetoa msimamo mpya kuhusu matokeo ya uchaguzi huo.

Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa endapo wagombea wake wote ikiwa ni pamoja na mgombea urais Maalim Seif Sharif Hamad watashinda katika uchaguzi huo, hawatakubaliana na matokeo hayo.

Alisema kwakuwa ZEC wameendelea kuyaweka majina ya wagombea wake kwenye karatasi za kura licha ya kuwaandikia barua rasmi ya kujiondoa katika uchaguzi huo, kuna uwezekano baadhi ya majimbo yakatangazwa kuwa yamechukuliwa na CUF. Alisisitiza kuwa endapo hilo litatokea wagombea wake wote hawataenda kuapishwa.

“Hata kama wananchi watamchagua Maalim Seif kwa asilimia 90 hawezi kwenda kuapishwa. Kufanya hivyo ni sawa na kukataa kula nyama ya nguruwe lakini unakunywa mchuzi wa nyama hiyo,” alisema Mazrui.

Alisema tayari wamepeleka ZEC barua 54 za wagombea wao nafasi za wawakilisha na udiwani walioshinda na walioshindwa katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana. Hata hivyo, ZEC imeendelea kuweka kuweka orodha ya wagombea waliotangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu.

ACT Wazalendo walia na Magufuli, Wakosoa jitihada za mabadiliko ya Mfumo
Sababu 3 muhimu, Kwanini hupaswi kufanya ngono siku ya Valentine