Kocha wa Yanga Hans van Pluijm na Stewart Hall wa Azam walizungumzia mchezo wa jana kila mtu kwa wakati wake huku kila mmoja akisema mchezo huo ulikuwa mgumu, wenye ushindani wa hali ya juu na ulistahili kuwa mchezo wa fainali ya Kagame.

Pluijm amesema baada ya kutupwa nje ya mashindano hayo sasa mipango yake anaihamishia kwenye maandalizi ya ligi kwa ajili ya msimu ujao wa 2015-2016.

“Dakika 45 za kwanza hatukuwa vizuri kwenye mchezo, lakini nafikiri kipindi cha pili tulicheza vizuri sana. Dakika za mwisho kama tungetumia vizuri nafasi tulizotengeneza tungeibuka na ushindi lakini kupoteza mechi kwa namna hii inaumiza sana”, Pluijm alisema.

“Tulijifunza kupiga penati siku moja kabla na kila mtu alifunga penati lakini hii ilikuwa kama ni fainali. Kama unapata nafasi ya kucheza mashindano kama haya halafu unacheza nyumbani unakuwa tayari kubeba kombe lakini kwa bahati mbaya haijawa hivyo”, aliongeza.

“Sasa kilichobaki ni kujiandaa na msimu ujao wa ligi na hicho ndicho kilichobaki”, Pluijm alimaliza.

Kwa upande wa kocha wa Azam Stewart Hall yeye alisema, mchezo ulikuwa ni waushindani mkubwa ambapo wachezaji walicheza kwa nguvu na kuongeza kwamba mchezo huo ulitakiwa uwe ni wa fainali ya michuano hii.

“Mchezo ulikuwa ni wa ushindani mkubwa na wachezaji walicheza kwa kujituma” Alisema Stewart

Maradona Amtuhumu Mkewe Kumuibia Fedha Zake
Man Utd Wachezea Kichapo Marekani