Masaa machache yaliyopita zilisambaa picha zinazoonesha Mkutano Mkuu wa Chadema uliohudhuriwa na viongozi wote wa ngazi za juu wa chama hicho, huku aliyekuwa waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa akionekana kwenye meza kuu ya kikao hicho hali inayoashiria wazi kuwa amejiunga rasmi.

Picha hizo zisizokuwa na maelezo ya kutosha japo lugha ya picha inatoa maelezo ya jumla, zilipata maelezo mbalimbali na kuzua mjadala mrefu kwenye mitandao ya kijamii.

Baadhi ya wanasiasa wakubwa tayari wameshatoa maoni yao huhusu picha hizo na tukio zima linaloashiria kuwa Edward Lowassa amehamia rasmi katika Chama Cha Demokrasia na Maendeo (Chadema).

Naibu Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, January Makamba, kupitia tweeter ameeleza kuwa hatua hiyo imerahisha zaidi kazi ya CCM kwenye uchaguzi mkuu.

“The election just got easier for CCM,” ametweet Makamba masaa machache baada ya tukio hilo kuonekana kwenye mitandao.

 

Naye kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amepost picha hizo kwenye mitandao ya kijamii nakueleza kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 unavutia. “It is offficial. CHADEMA central committee welcomes ex premier Edward Lowasa. 2015 very exciting elections.”

Maria Sarungi, mwanaharakati ambaye ni mwanaharakati mwenye ushawishi wa kati kwenye mtandao wa Twitter na anaefahamika zaidi kwa kuendesha mijadala kwenye mtandao huo, kabla ya kuandika tweets zinazowataka watu wasubiri kusikia tamko rasmi la Chadema, alitweet:  

Tweet ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dr. W. Slaa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, ilikuja kwa mfumo tofauti na wengi waliokuwa wanaufikiria. Slaa ambaye aliwahi kuwa Padre wa Kanisa Katoliki, aliweka fumbo kwa kunukuu kifungu cha Biblia kinachoweza kukuunganisha moja kwa moja na tukio hilo. 


Hata hivyo, kabla picha hizo hazijasambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alitweet jina la ‘LOWASSA’ kwa herufi kubwa kama nilivyoandika na baadae kupost picha inayomuoesha akiwa na mbunge huyo wa Monduli, masaa matano kabla picha hizo hazijasambaa mitandaoni.

Awali, baadhi ya wabunge wa Chadema waliwahi kueleza nia ya kumpokea Edward Lowassa katika chama chao baada ya kuwepo tetesi nyingi za mwanachama huyo wa zamani wa CCM kukihama chama hicho.

Taarifa zinaeleza kuwa Lowassa atatambulishwa rasmi kesho kama mwanachama wa Chadema na huenda akawa ndiye aliyepewa jukumu la kupeperusha bendera ya Ukawa kwenye uchaguzi mkuu akiwania nafasi ya urais.

Edward Lowassa aliondolewa katika kinyang’anyiro cha uraisi kupitia CCM, uamuzi ambao yeye na timu yake uliupinga na kudai kuwa ulifanywa kwa maslahi ya baadhi ya viongozi wa Chama hicho.

Stevan Jovetic kuitosa Man City
Ramos aitikisa Real Madrid