Watu nane wakiwamo walimu wanne wa shule ya msingi Bulyahilu katika Kata ya Ilingamba Halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema, Mwanza wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa mitihani ya darasa la saba inayoendelea.

Hayo yamethibitishwa leo Septemba 6 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana ambaye amethibitisha kutiwa mbaroni kwa watuhumiwa hao na kwamba uchunguzi unaendelea kubaini namna walivyojihusisha wizi wa mtihani wa somo la Kiswahili.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bahebe Kidesheni, wasimamizi watatu wa mitihani pamoja na mgambo aliyekuwa akilinda usalama wakati wa mitihani shuleni hapo .

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa walimu hao waliuiba mtihani wa Kiswahili na kwenda kujifungia mahali kisha kuufanya kwa ajili ya kuwapa wanafunzi majibu.

 

Adam Lallana nje majuma manne
Akili za Gigy, ona anachowaza kukifanya na mtoto wa Zari