Wizara ya Elimu nchini imeahidi kusambaza kompyuta mpakato kwa walimu 400 kila mwaka, kwa ajili ya kusaidia kupata uelewa wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) na kuwarahisishia kazi zao.

Hatua hiyo imebainishwa katika maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani yaliyofanyika katika wilaya ya Gasabo na kuhudhuriwa na walimu wa wilaya hiyo na viongozi mbalimbali wa serikali.

Waziri wa Nchi anayeshughulikia Elimu ya Msingi na Sekondari, Isaac Munyakazi, amesema hatua hiyo ni sehemu ya mikakati ya serikali katika kuimarisha mitaala ambapo Tehama ikiwa ni muhimu kusaidia walimu kupata uelewa utakaosaidia wanafunzi.

“Wanafunzi hawawezi kupata uelewa na masomo hayo ikiwa walimu hawana uelewa wake, katika miaka michache iliyopita tuliweka mkazo kwa wanafunzi, lakini sasa tunataka walimu na wanafunzi kwenda sambamba kupata elimu hiyo,” alisema.

Aidha, amesema kwa kuwawezesha walimu katika matumizi ya teknolojia hatimaye wanafunzi watanufaika na elimu hiyo, lakini kutokana na changamoto ya kifedha, wizara haitaweza kusaidia walimu wote kwa wakati mmoja. Katika maadhimisho hayo, walimu walitaka serikali kuangalia upya mishahara yao kutokana na viwango vya maisha vya sasa, hivyo serikali kuahidi kufanyia kazi suala hilo

Abiria wa Ukerewe wagoma
Video: Iokote ya Maua Sama yashika kasi, Vanessa aja kivingine