Walimu wametakiwa kuzingatia maadili wanapokuwa kazini na kuhakikisha wanaweka kando mitindo ya urembo na mavazi yasiyofaa kazini ikiwa ni pamoja na kupaka wanja na rangi midomoni (lipstick).

Hayo yamesemwa na Afisa Utumishi wa Wilaya ya Geita, Thabitha Bugema alipokuwa anazungumza na walimu wakuu na waratibu wa elimu wilayani humo wakati akitoa muongozo kuhusu matumizi ya fedha za kuwezesha elimu bure zilizotolewa na serikali.

“Nashindwa kuelewa wapo walimu wanavaa kama wauza baa, amejipaka lipstick (rangi ya mdomo) na wanja kama anakwenda kwenye kumbi za muziki usiku, wakuu wa shule sitegemei kuwaona mkifumbia macho walimu wa aina hiyo,” alisema Bugema.

Alisema kuwa wapo walimu wa kiume ambao kwa makusudi huingia shuleni wakiwa wamevaa jeans na wengine wakiwa wamevaa suruali chini ya makalio (mlegezo), kinyume cha maadili ya utumishi wa umma. Aliagiza wakuu wa shule kuhakikisha wanawachukulia hatua stahiki.

 

Mahakama yafuta kesi dhidi ya kafulila
Walichozungumza Maalim Seif, Lowassa na viongozi wa Ukawa kuhusu Zanzibar