Miili ya watu wa watano kati ya sita waliofariki dunia katika ajali ya basi dogo la abiria lililogongana na lori eneo la Mzibira Kata ya Uyovu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita imetambulika huku Mganga Mkuu Wilaya ya Bukombe, Dkt. Deograsia Mkapa akitaja majina ya marehemu.

Amesema, waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea alfajiri ya Julai 13, 2023 ni Dereva wa basi hilo aina ya Toyota Hiace, Habib Abeid (27) kondakta wake Aziz Omari (25), Daniel James (27), Innocent John (25) na Magigi Shitabu (60) na maiti ya mtu mmoja haijatambuliwa.

Lori lililogongana na Basi hilo dogo la abiria.

Aidha, Dkt. Mkapa amewataja majeruhi wawili wa ajali hiyo kuwa ni Jackson Wizeye Joseph (38) na Wilson Daniel (49), wote wakazi wa Ngara mkoani Kagera ambao awali walikimbizwa katika Hosipitali ya Uyovu kabla ya kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa gari dogo la abiria kusinzia wakati gari, likiwa kwenye mwendo kasi likiwa linatokea Kahama kuelekea Nyakanazi.

Dkt. Mwinyi akemea urasimu kwenye biashara
Luis Enrique kuitega Atletico Madrid