Hatua ya makundi ligi ya wanawake Tanzania Bara ilihitimishwa jana  na timu nane kutoka vituo vyote viwili vya Arusha na Dar es Salaam zitaingia kwenye hatua ya nane bora ‘Super Eight’ ambayo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Timu zilizofunzu kutoka kundi A ni vinara JKT Queens, Mlandizi Queens, Ever Green pamoja na Simba Queens zote za Dar es Salaam, wakati kutoka kwenye kundi B ni Sister FC ya Kigoma, Alliance Queens ya Mwanza, Panama FC ya Iringa na Marsh Athletics ya Mwanza.

Majengo Queens ya Singida na Mburahati Queens ya Dar es Salaam zimeporomoka daraja.

Msuva: Sitamani tupangwe dhidi ya Yanga
Kili Stars kukamilisha ratiba, kocha apania kuondoka na point