Wanasayansi wawili, Kataline Kariko na Drew Weissman ambao waligundua chanjo za Covid aina ya mRNA, wameshinda Tuzo ya Nobel ya Dawa ya mwaka 2023 ambayo huwa ya kwanza kutolewa miongoni mwa nyingine za kila mwaka.
Kamati ya tuzo hizo, imesema Wanasayansi hao Kariko ambaye ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Szeged na Chuo cha Afya cha Perelman Pennsylvania na Weissmana ambaye ni Profesa wa Chuo cha Utafiti wa Chanjo cha Roberts Family na Mkurugenzi wa Chuo cha RNA Innovations cha Pennsylvania walipiga hatua muhimu.
Tuzo za fizikia, kemia, fasihi, amani na uchumi zitatangazwa kila siku hadi Okotoba 9, 2023 ambapo mwanzilishi wa tuzo hizo, Alfred Nobel alikuwa ni Mfanyabiashara katika karne ya 19 aliyejipatia utajiri mkubwa baada ya kugundua dynamite, huku Tuzo ya kwanza ya Nobel ikitolewa mwaka 1901 ikiwa ni miaka 5 baada ya kifo chake.