Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameridhia Watumishi walioondolewa kazini kwasababu ya kughushi vyeti warudishiwe michango yao waliyochangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
Hayo, yamesemwa hii leo Oktoba 26, 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Prof. Joyce Ndalichako na kuongeza kuwa michango hiyo ni ile ya PSSSF ni asilimia 5 na NSSF ni asilimia 10 ya mshahara wa muhusika na isiyohusisha malipo mengine ya ziada.
Amesema, marejesho ya michango kwa Watumishi hao yataanza kufanyika kuanzia Novembea mosi, 2022 ambapo mtumishi atatakiwa kufika kwa aliyekuwa Mwajiri wake akiwa na nyaraka muhumu.
Nyaraka hizo ni pamoja na kitambulisho, nakala za kibenki na passport size ili kumuwezesha kutambulika kwa urahisi wakati wa uhakiki wa taratibu za malipo.