Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imesema kuwa inafuatilia kwa ukaribu tuhuma zinazotolewa dhidi ya wabunge waliohama vyama vyao kuhusu kujihusisha na rushwa.

Kauli hiyo ya Takukuru imekuja katika wakati ambao si tu wapinzani bali jamii na baadhi ya wabunge kugubikwa kuwa wanasiasa hao wanaohama kutoka upinzani kwenda chama tawala wanapewa rushwa, huku nia kubwa ikiwa ni kudhoofisha upinzani.

Aidha, Msemaji wa Takukuru, Musa Misalaba amekiri kusikia taarifa hizo kupitia kwenye mitandao ya kijamii na kusisitiza kuwa wao kama Taasisi wako makini na wanafuatilia mahala popote penye harufu ya rushwa.

Hisia zimetawala zaidi baaada ya wabunge wawili wa upinzani waliokuwa wanaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliyekuwa mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtulia na Godwin Mollel aliyekuwa mbunge wa jimbo la Siha kupitia tiketi ya Chadema kuhamia CCM.

Hata hivyo, mbali na wabunge hao kuhamia CCM, wengine ni pamoja na aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bavicha, Patrobas Katambi.

 

 

Zuma awatahadharisha wafuasi wa ANC
Video: Mfungwa aliyesamehewa na JPM afungwa miaka 15, NHC moto