Wananchi nchini Syria waliokuwa wanaishi kwa kula nyasi na udongo katika mji wa Madaya huku miongoni mwao wakifa kutokana na kukosa chakula wameanza kupewa misaada.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa serikali ya Syria imeanza kuruhusu kupelekwa misaada ya kibinadamu katika mji huo uliokuwa umezingirwa na uliokuwa umekaliwa na waasi karibu na mpaka wa Lebanon.

Picha za video zilikuwa zilionesha mji huo uliokuwa umezingirwa na majeshi ya serikali na wafuasi wa Hezbollah kwa miezi kadhaa, zilonesha wakazi wa maeneo hayo wakiwa katika hali mbaya na waliodhoofu miili.

Grey Barrow, Mkuu wa shirika la Chakula duniani amesema kuwa wanafanya jitihada za kuhakikisha watu wote wanaohitaji msaada katika mji huo wanafikiwa na kuhudumiwa.

Diamond atajwa tena tuzo kubwa Afrika
Mtuhumiwa namba Moja Kesi Ya Mauaji ya Dk. Mvungi Afariki