Watu 44 wamefariki dunia baada ya kunywa pombe yenye sumu kwa imani kuwa inaweza kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Msemaji wa Iran amesema tukio hilo limetokea baada ya baadhi ya watu kusambaza imani potofu na kusababisha watu 331 kunywa pombe hiyo.
Unywaji wa Pombe umepigwa marufuku nchini humo isipokuwa kwa wachache wasio Waislamu, lakini mara kwa mara kumekuwa na ripoti za watu kunywa pombe yenye sumu.
Virusi hivi vinaendelea kusambaa duniani na mataifa yaliyoathiriwa zaidi ni China, Korea Kusini, Italia, Iran, Ufaransa na Ujerumani.