Wakimbizi waliopewa uraia wa Tanzania wametakiwa kuacha kuitumia vibaya nafasi hiyo kwa kuingiza watu wengine  kinyume cha sheria kwani wakifanya hivyo watanyang’anywa na kurudishwa walikotoka.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wakati akizungumza na waliokuwa wakimbizi wa Burundi ambao kwa sasa wamepewa uraia wa Tanzania wanaoishi katika Kata ya Katumba, Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mpanda.

Pia, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini wawe wanawaelimisha waumuni wao umuhimu wa kulinda amani na kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi husika.

“Wakimbizi waliopewa uraia wameendelea kuingiza ndugu zao. Naagiza kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ifanye ukaguzi katika kambi zote kwa sababu zimegeuzwa kuwa maficho ya kuwahifadhi watu wanaoingia nchini bila ya vibali,” – Majaliwa

Majaliwa ameitaka kamati ya ulinzi ya mkoa Katavi kuhakikisha inachukua hatua kwa wote watakaoingiza watu kinyemela katika kambi za wakimbizi za Mishamo na Katumba. Pia amewataka wasiruhusu watu kuleta silaha kwenye maeneo haya. “Tanzania watu wanaoruhusiwa kutembea na silaha ni askari tu,” Majaliwa

Waziri Mkuu amesema lazima ulinzi uimarishwe katika maeneo ya mipakani na wasipofanya hivyo watu wengi wataingia nchini bila ya kuwa na vibali hivyo kusababisha ongezeko kubwa la idadi ya watu.

Picha: Ziara ya Waziri Mkuu Inyonga, Milele
Mbowe: Tutawaeleza wanachama kusitisha mikutano ya Septemba 1…