Mkurugenzi wa Lucky Vicent, Innocent Mushi na Makamu Mkuu wa shule hiyo, Longino Vicent wamehukumiwa leo Juni 10, 2019 baada ya kukutwa na hatia ya makosa 5 yaliyosababisha kutokea kwa ajali ya iliyopoteza maisha ya wanafunzi, walimu pamoja na dereva.

Ambapo Mushi amehukumiwa jela miaka 4 na miezi 6 au kutoa faini ya shilingi milioni moja na nusu huku Longino yeye amehukumiwa jela mwaka mmoja au kutoa faini ya Shilingi laki 5.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya hakimu Mkazi Arusha kufuatia ajali ya gari iliyotokea Mei 6, 2017 na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja.

Hakimu aliyewasomea mashtaka hayo na ametaja makosa 5 yanayowakabili wakuu hao wa shule ikiwa ni pamoja na kuvunja sheria za usalama barabarani, kuendesha gari za abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, gari lililosababosha ajali kutokuwa na bima, kushindwa kuingia mkataba baina ya dereva na mwajiri na kosa la kuzidisha abiria 13 katika gari lililopata ajali.

Aidha ajali hiyo  iliyotokea Mei 6, 2017 katika eneo la Rhotia wakati wanafunzi wa shule hiyo wakitoka Arusha majira ya saa 12 asubuhi kwenda wilayani Karatu katika mtihani ya ujirani mwema katika shule ya Tumaini Academy.

Waziri Dkt. Mpango amfunda kamishna mpya wa TRA,
Naipongeza BHATI AIRTEL. wamekuwa Wazalendo- JPM