Jeshi la polisi nchini Marekani linawashikilia wanaume wanne wanaoshukiwa kuhusika na kifo cha muigizaji maarufu Michael K. Williams aliyefariki kwa kile kilichotajwa kuwa alizidisha matumizi ya dawa za kulevya hadi kufikia hatua ya kupoteza maisha.

Kwa mujibu wa mkaguzi wa kimatibabu aliyebainisha kuwa kifo cha nyota huyo kilisababishwa na athari zilizotokana na kuzidiwa na dawa za kulevya aina ya heroini na cocaine.

Maafisa wa polisi waliwakamata washukiwa hao, ambao inadaiwa walikuwa sehemu ya wafanyakazi wa genge la ulanguzi wa dawa za kulevya huko Brooklyn, na wametiwa mbaroni kwa madai ya kumuuzia marehemu Williams dozi hiyo hatari huku ya wakifahamu undani wa athari zitokanazo na dawa hizo.

Wakili Damian Williams amesema kuwa video ya uchunguzi ilinasa matukio kadhaa ya kutumiana dawa za kulevya kati ya Williams na Irvin Cartagena ambaye ni mmoja wa watuhumiwa hao, siku moja kabla ya kifo cha nyota huyo.

Watuhumiwa wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani ni Hector Robles, 57, Luis Cruz, 56, na Carlos Macci, 70 pamoja na Irvin Cartagena.

Michael K. Williams alifariki Dunia, Septemba 25 mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 54 ambapo mwili wake ulipatikana katika nyumba yake huko Manhattan nchini Marekani.

Saratani yaongezwa na mtindo wa maisha
Chozi la CEO wa Facebook Mack Zuckerbeg