Wakati dirisha la usajili likiwa limefungwa usiku wa jana huku baadhi ya vilabu vikifanikiwa kufanya usajili dakika za lala salama, kuna baadhi ya madili yamekwama dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa usajili huo wa January.

Yafuatayo ni baadhi ya majina ya wachezaji walioshindwa kujiunga na vilabu vilivyoonesha nia ya kuwahitaji kabla ya dirisha hilo la usajili halijapigwa kufuli.

Saido Berahino kutoka West Brom kwenda Newcastle

Berahino

Mchezaji Saido Berahino wa West Brom alikuwa akiwaniwa na vilabu kadhaa lakini bado dili lake lilikwama hadi dirisha la usajili linafungwa.

Tottenham walipeleka offer ya £22.5m wakati wa majira ya kiangazi lakini wakapigwa chini na klabu hiyo. Jumapili Newcastle wakaenda na offer ya £21m lakini pia wakatolewa nje.

Alex Teixeira kutoka Shakhtar Donetsk kwenda Liverpool

Alex Teixeira

Liverpol nao wakakwama kumsajili mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk Alex Teixeira mwenye umri wa miaka 26. Majogoo hao wa jiji walikuwa na kitita cha £24.5m kwa ajili ya striker huyo wa kibrazil lakini klabu yake ya Ukraine ilikuwa ikitaka dau la £39m ambalo liliwashinda Liverpool na kuachana na mchezaji huyo.

Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwenda Leicester City

Musa

Kikosi ambacho kipo kwenye mbio za kuwani ubingwa msimu huu Leicester City kilitoa offer ya £18.7m kwa ajili ya kumnasa forward wa CSKA Moscow Ahmed Musa lakini hawakufikia muafaka na klabu yake iliyokuwa ikitaka £22.8m kutokana na kipengele cha kumuuza mchezaji huyo kilichopo kwenye mkataba wake.

Lakini pia walishindwa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea Loic Remmy.

Radamel Falcao kutoka Chelsea kwenda Atletico Madrid

Falcao-Chelsea

Imeripotiwa kwamba, kikosi cha Chelsea kilikuwa kinatarajia mshambuliaji wake raia wa Colombia Radamel Falcao huenda angeondoka kwenye kikosi hicho baada ya kuwepo Stamford Bridge kwa mkopo lakini dili la kutimkia Atletico Madrid halikufanikiwa.

Arsene Wenger Aanza Kuwazungumzia FC Barcelona
Wasaka Nyoka Tanzania Bara Kuumana Tena Kesho