Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dare es Salaam leo Septemba 11,2020 imewahukumu watu wawili Masse Uledi (43), na Nkinda Shekalage (34), kulipa fidia ya shilingi Milioni 16, baada ya kukiri kutumia jina la Janeth Magufuli kutapeli.

Pia Mahakama imewahukumu kutumikia kifungo cha nje cha miezi saba, kwa masharti ya kutotenda kosa lolote la jinai kwa muda huo.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando amesema mahakama inawataka washitakiwa kulipa fidia ya kutaifisha vifaa walivyokuwa wakivitumia kufanyia utapeli huo, ambavyo ni simu 12, kompyuta mpakato mbili, flashdisk tatu na modem mbili kuwa mali ya serikali.

Washitakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na makosa matatu, likiwemo la kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 12, 2020
Ujerumani,Urusi kushirikiana uchunguzi sakata la Navalny