Jaji wa Mahakama Kuu Nchini Marekani, anatarajia kuwahukumu wanachama wengine wawili wa kundi lenye msimamo wa mrengo wa kulia la Proud Boys ambao walivamia Bunge Januari 6, 2021 kutaka kuzuia kurasmisha ushindi wa Rais Joe Biden wakati wa uchaguzi.

Mshitakiwa wa kwanza wa Proud Boy ambaye atahukumiwa ni Dominic Pezzola, asiyekuwa na jukumu la uongozi katika kundi hilo na alikuwa ni mshtakiwa pekee kati ya watano asiyepatikana na hatia ya kushiriki katika njama za uchochezo huo.

Pezzola alitiwa hatiani kwa makosa mengine ikiwa ni pamoja na kuingilia kati shughuli rasmi na kuwashambulia polisi. Mshtakiwa wa pili, Ethan Nordean, alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambaye alikutwa na hatia za kula njama za uchochezi na uhalifu mwingine.

Maelfu ya wafuasi wa Trump walilishambulia jengo la Bunge (Capitol), kufuatia hotuba ya chama cha Republican ya tuhuma za uongo kwamba kushindwa kwake katika uchaguzi wa Novemba 2020 kulitokana na udanganyifu ulioenea, ambapo Watu watano akiwemo afisa wa Polisi walifariki wakati au muda mfupi baada ya ghasia hizo, huku zaidi ya maafisa 140 wa Polisi wakijeruhiwa.

Middendorp akabidhiwa mikoba Singida FG
Rais Samia kufungua Mkutano Maafisa wa Polisi