Serikali imewatimua wananchi ambao walivamia shamba la Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ritha Mlaki.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki amewataka wananchi hao zaidi ya 2000 ambao wamebainika kuwa baada ya nyumba zao kubomolewa katika maeneo yasiyofaa kuwa makazi na kisha kuamua kuvamia mashamba hayo kuondoka mara moja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

“Kisa wamebomolewa nyumba zao walizojenga kinyume na sheria ndio wavamie maeneo yasiyo yao, hili ni kosa kama makosa mengine. Nawataka watoke haraka vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema Meck Sadiki.

Awali, Sumaye aliwaambia waandishi wa habari kuwa hana wasiwasi kutokana na wananchi hao kuvamia shamba lake kwakuwa anajua analimiliki kisheria hivyo vyombo husika vingemrudishia haki yake.

 

Serikali: Hakuna Viwanja vya Kuwagawia waliobomolewa Mabondeni
Picha: Mwanamke mrembo achinjwa kwa kuipinga ISIS