Wakati Kampeni ya kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Ini ikiendelea Zanzibar, takwimu zimebainisha kuwa watu waliozaliwa kabla ya mwaka 2005 wana hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Ini, kwani chanjo ya ugonjwa huo hapa nchini ilianza kutolewa kwa watoto waliozaliwa mwaka 2005.
Akizungumza katika kampeni ya kukabiliana na ugonjwa wa Ini, Meneja wa kitengo shirikishi cha UKIMWI, homa ya Ini, kifua kikuu na Ukoma Zanzibar, Johari Khalid amesemakuwa kuna chanjo ya ugonjwa huo ambayo ilianza kutolewa mwaka 2005 kwa lengo la serikali kuona inakabiliana na ugonjwa huo.
Takwimu zinaonesha kuwa watu 357 wamegundulika kuambukizwa homa ya ini ‘B’ kuanzia mwaka 2005 hadi hivi sasa katika kliniki ya Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzibar, kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa kwa miaka minane umebaini maambukizi ya homa hiyo upande wa wanawake ni 127 na wanaume 230.
Aidha, Johari ametaja baadhi ya sababu za maambukizi hayo kuwa ni kufanya ngono isiyo salama, kuingiziwa Damu na kujidunga sindano hasa kwa wale watumiaji wa dawa za kulevya. na watu ambao wana athirika zaidi na ugonjwa huo ni wenye umri kuanzia miaka 20 ambao tayari wameanza kukabiliana na Mazingira nyemelezi ambayo mara nyingi huishi kirusi wa maradhi ya Hepatitis B.
-
JPM afanya uteuzi mwingine
-
Serikali kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Takwimu
-
Dereva wa lori adaiwa kuiba pipa 156 na kutoroka
Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado kuna haja na dhima kwa jamii kuchukua tahadhari zaidi ya kujikinga kwa kuepukana na kufanya ngono zembe,kuchangia Damu ambayo haija pimwa, na kuepuka kuchangia sindano, kwani homa ya Ini ni ugonjwa hatari kama yalivyo maradhi mengine kama UKIMWI,Kifua kikuu na Kipindupindu